KIBOSHO SEMINARY ONLINE MEDIA

@kiboshoseminaryonlinemedia ni jukwaa la mtandao wa Youtube (pia tuna majukwaa ya facebook, instagram na WhatsApp) yaliyoanzishwa na uongozi wa Seminari kuu ya Mama Bikira Maria Malkia wa Malaika - Kibosho kwa lengo la kuhabarisha na kuelimisha hadhira wa ndani na nje ya Seminari. Katika jukwaa hili utapata habari na matukio ya Seminari yetu pia Vipindi vyenye maudhui ya Kikatoliki ikiwemo vipindi vya Sala, Nyimbo, Masomo ya Misa, Tafakari za wiki na Dominika pamoja na Historia za Maisha ya Watakatifu.