Amatha K. Mwapinga(Beloved)

Muziki Mtakatifu, Documentary za watunzi wa muziki Mtakatifu na mada zinazohusu wanautume na Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania(UKWAKATA)

🟣YbSira 2:1–6
"Mwanangu, ukija kumtumikia Bwana, weka tayari roho yako kwa kujaribiwa. Ujitengeneze moyo ustahimili, wala usitaharuki siku ya kuteswa.Uambatane naye wala usijitenge tena, ili mwisho wako ukuzwe. Kila utakalopelekewa ulipokee kwa kuchangamka moyo, uyavumilie mabadiliko ya unyonge wako.Maana dhahabu hujaribiwa motoni, na watu wateule kalibuni mwa unyonge.

🟣1 Petro 3:16–17
"Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya"

🟣1 Timotheo 1:12
"Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;"

🟣Luka 17:10
"Mimi ni mtumwa nisiye na faida; nimefanya tu yaliyonipasa kufanya."