SAYUNI EAGT CHURCH

Kanisa la Sayuni EAG(T) Sinoni-Arusha, chini ya Askofu Dr. Leonard Mwizarubi pamoja na Dr. Amesario Leonard Mwizarubi linaamini katika kuongeza thamani ya maisha ya watu kwa kupitia mafundisho sahihi ya neno la Mungu.

Kwenye channel hii utapata mafundisho yatakayobadilisha maisha yako pamoja na shuhuda za matendo makuu ya Mungu kutokana na huduma ya watumishi wa Mungu Askofu Leonard Mwizarubi pamoja na Dr. Amesario Mwizarubi katika kanisa la Sayuni tangu miaka ya 1990.

Tunaamini kupitia mafundisho sahihi ya neno la Mungu na Roho mtakatifu mtu anaweza kuishi Maisha matakatifu akiwa hapa hapa duniani tofauti kabisa na fikra potofu kuwa hakuna utakatifu duniani “Zab 16:3”