UzimaTele TV

Pentecostal Holiness Mission (PHM),
Ni Kanisa ambalo linaloongozwa katika misingi ya Kipentekoste. Kanisa la PHM - UZIMA UKONGA, lipo Jijini Dar es Salaam, Ukonga - Magereza katika eneo la Kichangani - Madukani. Kanisa linaamini juu ya Ubatizo wa Maji Mengi, Wokovu kwa wanadamu wote unaopatikana kwa kumwamini YESU KRISTO MWANA wa MUNGU aliye HAI. Na pia tunaamini juu ya ROHO MTAKATIFU mwenye Nguvu na Uweza ambaye humpatia Nguvu na Uwezo wa Kuishi maisha Matakatifu na Ushindi kila aaminiye kwa mujibu wa Ahadi za NENO LA MUNGU.

Kanisa la PHM - UZIMA UKONGA , DAR ES ALAAM lipo chini ya uangalizi wa Mchungaji Dickson Sifaeli Mbwambo na Florence S Mbwambo ambaye pia ni Askofu Msaidizi wa Jimbo - Sehemu ya Temeke.

Mungu Mkuu Kwa Utukufu Wake anawatumia watumishi wake, Kurejesha Uzima wa Mungu katika maisha ya watu walioteswa na Ibilisi shetani.
Yohana 10:10 "...Mimi nalikuja ili wawe na UZIMA, kisha wawe nao TELE"

Kwa mawasiliano: Piga +255 714 774 329 au +255 716 944 424