RuYACC TV

RuYACC ni kifupi cha maneno Ruangwa Youth, Art and Cultural Centre(RuYACC) Ni kituo cha Vijana Sanaa na Utamaduni Ruangwa.Kituo kipo Mkoa wa Lindi Wilaya Ruangwa eneo la Matyatya karibu na Machimbo. yà Mchanga. Kituo kina lengo la kuibua na kuendeleaza vipaji vya vijana waliopo , Mtaani, Chuoni , Shuleni na maeneo mengine ,Sambamba na kutunza na kuurithisha Utamaduni wa Mtanzania kwa vizazi viliopo na vijavyo. RuYACC TV inakusudia kuwafikia vijana wengi duniani kote kwa lengo la kuelimisha, kuburudisha na kufundishana tamaduni mbalimbali ili kumfanya kijana ajue wapi ametoka , wapi alipo na wapi anakokwenda, kuthamini na kuendeleza Utamaduni na Sanaa za asili, Kutambua kuwa hakuna Utamaduni bora kuliko mwingine, Utamaduni ni utambulisho wa jamii husika hivyo tuulinde ili tusipoteze utambulisho wetu. RuYACC "KIPAJI NI MTAJI"