Namsifu Maduhu Mwita

Ni wewe Mungu ninakuimbia. Asante sana kwa kunisikia nikiongea na wewe kwa njia ya nyimbo. Pokea sifa na utukufu maana ni wewe uliye Mkuu. Wakati wengine wanasifu watu, majumba, mali na umaarufu wa dunia hii mimi nimechagua kuliinua juu jina Lako takatifu. Nisaidie kuuelekeza moyo na maisha yangu yote kwako.
Wasaidie na wengine wakisia nyimbo hizi ziwaguse kukuelekea wewe. Bado nakuhitaji usiondoke, kaa nami tuimbe pamoja.