Fresh TV Tanzania

KANUNI NA MUONGOZO

FRESH TV ni chombo cha habari kinachozingatia weledi na maadili yanayoongoza tasnia ya habari. Tumejikita katika kuripoti habari na matukio ya michezo, burudani, muziki, filamu, mitindo ya maisha na masuala ya kijamii. Tunazingatia misingi ya uhariri katika habari kwa kufuata yafuatayo:

1. Kuripoti habari za ukweli
2. Kusaidia kurekebisha taarifa zilizopotoshwa ili kuwapa ukweli wafuatiliaji wetu
3. Kufuata misingi ya habari kwa kuripoti habari zenye uwiano na kutoa fursa sawa kwa pande zote
4. Kujiepusha na udini, ukabila au mambo yoyote yanayoweza kusababisha uchochezi

Muongozo kwa wafuatiliaji (subscribers) wetu

1. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake
2.FRESH TV ina uhuru wa kufuta maoni yasiyo na maadili au yenye matusi makali
3. FRESH TV ina uhuru wa kupitia maoni kabla hayajaonekana na watu wote
4. FRESH TV ina uhuru wa kumzuia mfuatiliaji aliyekiuka masharti asiweze kuona habari zetu au kuweza kuweka maoni