JUKTAMKIZ

JUMUIYA YA KUIMARISHA TAALUMA NA MAADILI YA KIISLAMU ZANZIBAR (JUKTAMKIZ)
Hii ni Jumuiya iliyoanzishwa kwa lengo la kuunganisha, kuhamasisha, Kuimarisha na kuisaidia jamii kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali katika harakati za kupeleka mbele maendeleo ya wanajamii ili kujikomboa kiimani, kiutamuduni, kifikra, mawazo, mitazamo, kielimu, kiafya na kiuchumi ambapo hatimae kupata jamii iliyo bora.

#DHAMIRA:
Kuimarisha jamii kufuata mwenendo wa dini ya kiislamu kwa kustawisha uundaji endelevu wa masuala ya afya, mifumo ya elimu, ujuzi na kukuza ufahamu wa elimu ya dini ya kiislamu ili kuwezesha jamii hususan wanawake na vijana (wasichana na wavulana) kuwa na uhakika wa usalama, utulivu na kuleta tija.

#LENGO KUU:
Lengo kuu la Jumuiya ni kujenga ustawi wa maadili mema katika jamii ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kupeleka mbele juhudi na harakati za kusimamia maadili na maendeleo ya Jamii ya Kiislamu.