REACHING-OUT DESTINIES MINISTRY

REACHING OUT DESTINIES
Ni huduma iliyoanzishwa ikiwa na madhumuni ya kuwasidia Watu kufika hatima zao na kuondoa vikwazo vyote vilivowekwa kwenye njia zao kwa kutumia silaha ya Maombi.
Isaya 57:14
"Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Kiondoeni kila kikwazacho Katika njia ya watu wangu."

Huduma hii ni muunganiko wa wakristo kutoka katika madhehebu mbalimbali.
Ambao kwa umoja wetu tumekuwa tukitafuta Muda wa kuomba pamoja kujengena na kuhimizana katika safari hii ya ukristo.

Pia huduma hii imekuwa ikitunza WATUMISHI wanaofanyakazi katika mazingira magumu na pia kuwasaidia wahitaji.
Tumekuwa tukifanya makongamano na vipindi mbali mbali vya maombi online.