Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Afrika

Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Afrika, ni shirika la kwanza mno la utangazaji la kimataifa linalomilikiwa na wanahabari huru wa kimataifa wa Afrika, kupeperusha habari za kina na moto moto zinazogonga vichwa vya habari kote Afrika Mashariki na ya Kati, kwenye nchi za Maziwa Makuu, Upembe wa Afrika, na kote kote duniani.

Haya ni matangazo ya moja kwa moja ya dakika 30, yanayorushwa kuanzia 6:00-6:30 Asubuhi na Jioni kutoka 7:30-8:00, kila siku. Maudhui na msuko wa habari na vipindi vyetu unajumuisha vivutio vya majadiliano ya kina na wageni na wataalam. Vipindi vinaakisi maudhui mbalimbali kama vile siasa, teknohama, sayansi, michezo na burudani, afya, masuala ya vijana na wanawake pamoja na ujasiriamali. Pia, kila baada ya matangazo kuna tahariri ambayo inarejelea msimamo wa Afrika kuhusu matukio mbalimbali duniani.

Sikiliza mubashara matangazo yetu kupitia majukwaa yetu ya kijamii; Facebook Page na Youtube na Redio Washirika kote Afrika.