Sheikh Abdallah Saleh Al-Farsy

Darsa na mawaidha ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ‎رحمه الله aliyekuwa Chief Kadhi wa Zanzibar na Kenya, na aliyetafsiri Qur'ani kwa Kiswahili. Mtungaji wa vitabu vingi vya Kiislamu, mtetezi wa Sunnah ya Mtume ﷺ.

Amesema ‎رحمه الله: "...Kuna madhara makubwa kabisa ya duniani na Akhera katika kufuata dhana tu. Inataka kila unalolisema au kulifuata iwe una ujuzi nalo...Ilimu ya kweli ni: (a) Mwenyezi Mungu amesema, (katika Qurani); (b) Mtume amesema, (katika Hadithi zake Sahihi)" [Qurani Takatifu, uk. 733].