KMG TEGETA

Kwaya ya Mtakatifu Gaspar del Bufalo ni Chama cha kitume kinachohudumu katika Parokia ya Damu Takatifu ya Yesu - Tegeta, Dar es salaam.
Lengo letu ni kuhubiri na kumtukuza Mungu kwa njia ya nyimbo; Aidha shauku yetu kubwa ni watu wamjue Mungu wa pekee na kumtambua Yesu Kristo maishani mwao. Rejea Yohana 17:3

Mtakatifu Gaspar del Bufalo anasema...
"Kwa Mungu ni lazima tufanye mengi, upesi na vizuri...mengi kwa sababu anastahili hivyo ,upesi kwa sababu maisha ni mafupi na vizuri kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kumtumikia Mungu"