Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

RAIS SAMIA AHIMIZA USHIRIKIANO KUINUA TASNIA YA KAHAWA AFRIKA

Автор: MFA_Tanzania

Загружено: 2025-02-22

Просмотров: 175

Описание:

• Aahidi kuongeza bajeti ya kuendeleza sekta kilimo nchini
• Serikali kuongeza jitihada za kuongeza wigo wa soko la kahawa nje ya nchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezisihi nchi za Afrika zinazozalisha kahawa kushirikiana ili kukuza soko la kahawa na kufungua fursa za ajira kwa vijana barani Afrika.

Rais Samia ametoa rai hiyo alipozungumza katika Mkutano wa Tatu wa G25 wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazozalisha Kahawa uliofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Rais Samia amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kununua kahawa ya Afrika baada ya kuwa imeongezewa thamani kwa lengo la kukuza biashara ya kahawa miongoni mwa nchi za Afrika na hivyo kuimarisha sekta ya kahawa barani Afrika.

Mkutano huo, ulioendeshwa chini ya kaulimbiu isemayo "Kufungua Fursa za Ajira kwa Vijana Kupitia Uendelezaji wa Sekta ya Kahawa Afrika," uliwaleta pamoja viongozi kutoka nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa, wataalamu wa sekta ya kahawa na wawekezaji ili kujadili njia za kufufua sekta ya kahawa barani Afrika.

Rais Samia amesisitiza dhamira ya Tanzania ya kuongeza uzalishaji wa kahawa, kukuza biashara ya kahawa, kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la kahawa na hivyo kukidhi mahitaji ya soko.

Amesisitiza pia umuhimu wa kutokusafirisha kusafirisha kahawa ghafi na kuwekeza katika viwanda vya usindikaji wa ndani ili kuongeza mapato na kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania. "Lazima tukubaliane hapa, kahawa inayozalishwa Afrika inapaswa kusindikwa hapa hapa Afrika na kisha iuzwe nje ya bara hili, kuendelea kusafirisha kahawa ghafi ni kuuza ajira ya vijana wa Afrika nje ya bara, kuua soko la Kahawa na kuua mioyo ya wakulima kwani hawaoni manufaa ya kazi zao," alisema.

"Afrika inazalisha baadhi ya kahawa bora zaidi duniani, lakini bado tunabaki kuwa wauzaji wakuu wa Kahawa ghafi. Tunapaswa kubadilisha hali hii kwa kuhakikisha kahawa inayozalishwa Afrika inaongezwa thamani hapa hapa katika bara la Afrika, na kuimarisha biashara ya kikanda, na ndipo iuzwe nje ya bara la Afrika" amesisitiza.

Rais Samia pia ameeleza kuwa ushirikishwaji wa vijana katika sekta ya kahawa ni muhimu ili kuendeleza sekta hiyo na alizihimiza nchi za Afrika na wadau wa sekta hiyo kuwekeza katika programu za mafunzo, kutoa pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa kuwapa miche ya kahawa, mbolea na dawa za kuua wadudu pamoja na mbinu za kilimo za kisasa ili kuvutia vijana katika kilimo cha kahawa na usindikaji.

Rais Samia amesema kuna haja ya kuifanya Afrika kuwa soko kubwa la kahawa kwa kuhakikisha Kahawa inalimwa kwa wingi na kusindikwa barani Afrika.

Amesema Tanzania itaenda kutafuta soko la Kahawa iliyosindikwa ya Tanzania kwa mataifa mengine kama ya kutoka Mashariki ya Kati ambao alisema ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa kahawa duniani.

Alizisihi nchi za Afrika kukukubaliana kupitia Azimio la Dar es Salaam kuhusu Kahwa ambalo alisema kuwa linapaswa kuonyesha njia watakayoitumia nchi za Afrika ili kuwa soko kubwa la kahawa Duniani na jinsi watakavyofikia hatua hiyo na kuongeza kuwa uwepo wa soko la uhakika ndio jambo lka msingi.

Amesema Tanzania inalenga kuongeza uzalishaji na ubora wa kahawa ili kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa, kwa kuwawezesha vijana kushiriki katika kilimo kwa kuwapa miche na ruzuku ya mbolea. Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo tutakuza soko la kahawa na kuvutia vijana.

RAIS SAMIA AHIMIZA USHIRIKIANO KUINUA TASNIA YA KAHAWA AFRIKA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

WAFUGAJI TANZANIA KUNUFAIKA NA SOKO LA NYAMA NCHINI SAUDI ARABIA.

WAFUGAJI TANZANIA KUNUFAIKA NA SOKO LA NYAMA NCHINI SAUDI ARABIA.

FULL HISTORIA YA MAISHA YA MAMA SAMIA MPAKA KUWA KIONGOZI

FULL HISTORIA YA MAISHA YA MAMA SAMIA MPAKA KUWA KIONGOZI "NILIKATAA KUWA MAKAMU WA RAIS"

Fahamu maisha binafsi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Fahamu maisha binafsi ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Россия объявила срочную эвакуацию / Официальное заявление МИД

Россия объявила срочную эвакуацию / Официальное заявление МИД

KIJANA ANAYEIGIZA SAUTI YA RAIS SAMIA AWAVUNJA MBAVU MKUTANONI

KIJANA ANAYEIGIZA SAUTI YA RAIS SAMIA AWAVUNJA MBAVU MKUTANONI

RUTO IN TROUBLE! Kalonzo and ODM Set to Form a Formidable 2027 Alliance |Plug Tv Kenya

RUTO IN TROUBLE! Kalonzo and ODM Set to Form a Formidable 2027 Alliance |Plug Tv Kenya

Ijue familia ya Rais Samia Suluhu -mume, watoto na historia yake

Ijue familia ya Rais Samia Suluhu -mume, watoto na historia yake

Алиеву было «неудобно» приезжать в Петербург - декабрь, самолет

Алиеву было «неудобно» приезжать в Петербург - декабрь, самолет

Mahojiano Maalum na Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

Mahojiano Maalum na Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa

MAMA JASIRI AJILIPUA MBELE YA WAZIRI MKUU, SHERIA INAUZWA LAKI 5, KUNA WATU WAPO JUU YA SHERIA..

MAMA JASIRI AJILIPUA MBELE YA WAZIRI MKUU, SHERIA INAUZWA LAKI 5, KUNA WATU WAPO JUU YA SHERIA..

MWABUKUSI KIBOKO AMVAA RAIS SAMIA USO KWA USO

MWABUKUSI KIBOKO AMVAA RAIS SAMIA USO KWA USO "WATU WANATEKWA NA KUUAWA NA KESI HAZIELEWEKI

HOTUBA YA RAIS SAMIA  KWENYE BETHIDEI YA CHAMA CHA MAPINDUZI JAMHURI DODOMA

HOTUBA YA RAIS SAMIA KWENYE BETHIDEI YA CHAMA CHA MAPINDUZI JAMHURI DODOMA

Rais Magufuli ametaja mshahara wake leo

Rais Magufuli ametaja mshahara wake leo

IRELAND WAICHAGUA TANZANIA KUWA MAKAO MAKUU YAKE YA KIBIASHARA BARANI AFRIKA - MHE. THABIT KOMBO

IRELAND WAICHAGUA TANZANIA KUWA MAKAO MAKUU YAKE YA KIBIASHARA BARANI AFRIKA - MHE. THABIT KOMBO

Տերտերների անկողինը գերիներից կարևոր է|ԱՎԵԼԻ ԼՈՒՐՋ ՔԱՆ ԵՐԲևԷ

Տերտերների անկողինը գերիներից կարևոր է|ԱՎԵԼԻ ԼՈՒՐՋ ՔԱՆ ԵՐԲևԷ

CHEKI MLINZI wa RAIS SAMIA ALIVYORUKA KWENYE GARI - MSAFARA wa RAIS SAMIA UKIINGIA SABASABA...

CHEKI MLINZI wa RAIS SAMIA ALIVYORUKA KWENYE GARI - MSAFARA wa RAIS SAMIA UKIINGIA SABASABA...

MAONGEZI YA ANA KWA ANA KATI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA TIDO MHANDO

MAONGEZI YA ANA KWA ANA KATI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA TIDO MHANDO

RAIS MWINYI...TUNAWEZA KUIFANYA ZANZIBAR KUA SEHEMU SALAMA KWA .........

RAIS MWINYI...TUNAWEZA KUIFANYA ZANZIBAR KUA SEHEMU SALAMA KWA .........

UZINDUZI WA SERA YA MAMBO YA NJE 2001, TOLEO LA MWAKA 2024 - DAR ES SALAAM, TANZANIA

UZINDUZI WA SERA YA MAMBO YA NJE 2001, TOLEO LA MWAKA 2024 - DAR ES SALAAM, TANZANIA

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi,Moshi

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi,Moshi

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]