Historia_ya_Delcat_Idinco_by_PM_mtoto_wa_Henriette_[vidéo_officiel]
Автор: PM mtoto wa Henriette Officiel
Загружено: 2025-03-02
Просмотров: 10756
Hii ni historia ya mwana-mziki Delphin Katembo Vinywasiki maarufu DELCAT IDINCO.
Huyu DELCAT IDINCO alizaliwa tarehe 15/09/1993 huko beni.
Aliishi na familiya yake oicha mbele ya kuja kuishi katika muji wa beni.
Huyu alishuhudiya mauaji ya watu kuuwawa kama nyama huko beni.
Mauwaji ya kuchinjwa yaani kutenga mwili na kichwa, kupasua wamama wajawazito nakuuwa hadi mtoto ndani ya tumbo, na inasemekana baadhi ya familiya yake wamekufa kwenye haya mauwaji yanayo fanywa na waasi walio n'a jina maarufu NALU.
Hali hiyo ilimufanya kua mtetezi wa haki na usalama na kukanya uongozi mubaya wa viongozi(révolutionnaire).
zaidi alitetea sana watu kupitiya kipaji chake cha kupiga mziki.
Ali imba nyimbo za uhuru, nyimbo zakukanya viongozi kwa makosa yao, nyimbo za kuteteya wana inchi kwa haki zao, nyimbo zaku dénoncé viongozi...
Moja wapo ya hizo nyimbo ni(politicien escroc, Nikufe tu, président ashakimbiya...).
walimuita rafiki wa uhuru (Ami de la liberté) maana alitaka sana watu tuishi uhuru, na hilo jukumu lilifanya hadi serekali imuhukumu miaka kumi(10) jela tangu mwezi wa kumi na mbili mwaka wa elfu mbili makumi mbili na moja(12/2021).
Baadaye rahiya wakaandamana wakisema (awekwe huru Délicat Idinco!!!), na baada ya miaka mbili mwezi wa kumi na mbili mwaka wa elfu mbili makumi mbili na tatu(12/2023) aliwekwa huru DELCAT IDINCO.
Haikuishiya hapo
DELCAT IDINCO aliendelesha kazi yake ya kuteteya haki na usalama wa rahiya kupitiya nyimbo zake, ni hapo alipo anza tena na wimbo ulio kua na kichwa GUERIERS.
GUERIERS: ndani ya huu wimbo alitaka watu waelewe kwamba yeye ni shujaa na kwamba kila mumoja ni shujaa, na kutoa watu hofu ya kifo, hofu ya jela na kutaka watu wawe mashujaa wa kweli.
Ilipo timu tarehe makumi tatu mwezi wa mnane mwaka wa elfu mbili makumi mbili na ine(30/08/2024), ilisemekana kwamba Delcat Idinco amekamatwa tena akiwa katika harakati ya maandamano ya kutafuta haki ya wanainchi na uhuru.
Alisema hayo maneno Delcat idinco alipo tembelewa na CONGO CHECK ndani ya jela(prison) MUNZENZE pa goma tarehe makumi tatu mwezi wa kenda mwaka wa elfu mbili makumi mbili na ine(30/09/2024).
Sisi wazalendo wa congo DRC tukiwa tumejua kwamba yuko goma kwenye prison MUNZENZE, gafla ilipotimu siku ya ine saha za mchana tarehe kumi na tatu mwezi wa pili mwaka wa elfu mbili makumi mbili na tano, tukapata mushituko wa habari mbovu ya kwamba DELCAT IDINCO ameuawa sehemu za goma. (siku hiyo na saha zile alipo uawa DELCAT IDINCO kuna alama zilionekana, kubwa kati ya hizo alama ilikua Tetemeko kubwa ya inchi(tremblement de terre). Hiyo ndiyo historia halisi ya mwana mziki DELCAT IDINCO aliye zaliwa beni 15/09/1993 na akafia goma 13/02/2025.
Ni mimi mwanamuziki PM mtoto wa Henriette toka mjini Kirumba/territoire de Lubero/ Nord kivu DRC ndiye nimekutoleya hiyo adisi. Aksante kwa usomi usikose subscribe Chanel yetu
Adresse mobile:+243 990 608 839
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: