KUTOKWA/KUVUJA DAMU PUANI: Matibabu/Kujitibu mwenyewe nyumbani
Автор: WikiElimu
Загружено: 2025-03-06
Просмотров: 3747
Mishipa ya damu inayopita kwenye pua iko karibu sana, na unaweza kuiumiza kwa urahisi sana. Kwa watoto wadogo, kuchokonoa pua ni kawaida. Ni vizuri kuhakikisha kuwa kucha zao ni fupi na kuwazuia kuchokonoa pua, ukifanya hivi inaweza kusaidia kuzuia shida hii ya kutokwa damu puani.
Watu wengi wanatokwa damu puani kwa sababu ya mafua yanayosababishwa na virusi na kwa sababu ya kupuliza pua kwa nguvu. Tatizo kubwa zaidi hapa ni mafua, na kama mafua yakitibiwa vizuri inaweza kupunguza uwezekano wa kutokwa damu puani. Kama utando ute wa ndani ya pua umekauka, ni rahisi sana kupasuka na kusababisha damu kutoka.
Kumbuka mambo yafuatayo;
• Karibia nyakati zote, unaweza kuzuia damu inayotoka puani mwenyewe bila kuhitaji msaada wa mtu yoyote
• Kwa watu wengi, kutokwa damu kunaambatana na kuwa na mafua au kupata jeraha dogo kwenye pua
• Matibabu kama kuweka (pack) kitambaa au gauze ndani ya pua ili kuzuia damu kuvuja haisaidii na inapaswa kuepuka
• Mara nyingi kutafuta sababu ya kutokwa damu puani sio muhimu sana, kutafuta sababu kunaweza kufanyika hata baada ya damu kuacha kutoka
Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama unatokwa damu puani
Pua lina sehemu mbiili, sehemu ngumu inayotengenezwa na mfupa na sehemu laini kwa mbele. Sehemu ya pua ambayo kwa kawaida ndiyo huwa inavuja damu, ipo kwenye sehemu laini ya pua, na kwa kuibonyeza sehemu hii laini ya pua itasaidia damu kuacha kutoka.
Tumia kidole gumba na kidole cha kwanza kufinya sehemu ya mbele laini ya pua. Endelea kufinya kwa angalau dakika 5. Unapaswa kuwa umeketi ukiwa umeegea kwenda mbele. Usiegemeze kichwa kwenda nyuma. Ukiegemeza kichwa kwenda nyuma inasababisha damu kuvuja kwenda koo nah ii inaweza kusababisha ukapaliwa na itachukua muda mrefu zaidi kwa damu kukata. Kama una barafu karibu, ifunge kwenye kitambaa kicha iweke sehemu ya juu ya pua, baridi itasaidia mishipa ya damu kusinyaa na hivyo kuharakisha damu kukata.
Karibu matukio yote ya kuvuja damu puani yanweza kudhibitiwa kwa njia hii kama utashikilia pua kwa muda wa kutosha. Kama unaona damu haichi kutoka na unaona damu inatoka nyingi sana, Nenda kituo cha afya haraka upate matibabu ya dharura.
Matukio ya kutokwa damu puani, huwa yanaongezeka zaidi wakati wa baridi, kipindi ambacho watu wanapata mafua zaidi na upepo unasababisha pua kukauka. Unaweza kuzuia hali hii kwa kutumia vaporizer ndani ya nyumba yako ili kurejesha unyevunyevu – hii ni hasa kwa watu waoishi maeneo yenye baridi sana.
Kama kutokwa damu puani ni tatizo linalojirudiarudia, au unaona matukio ya kutokwa damu puani yanaongezeka na ukiangalia hayahusiani na baridi au kuchokonoa pua, ni vizuri pia ukamwona daktari ili akufanyie uchunguzi kutambua tatizo ni nini. Hauhitaji kwenda hospitalini moja kwa moja kama damu imekata, unaweza kusubiri. Maana unaweza kwenda kwa daktari na kwa sababu ya uchunguzi wake ukaanza kuvuja damu tena. Unaweza kwenda ahata siku nyingine, kama damu imekata.
JIFUNZE ZAIDI https://wikielimu.org
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: