🔴 RC RUVUMA ATOA SALAMU ZA POLE KIFO CHA MBUNGE JENISTA MHAGAMA
Автор: RUVUMA TV
Загружено: 2025-12-12
Просмотров: 127
Kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imetoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Jimbo la Peramiho.
Akizungumzia msiba huo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma umempoteza kiongozi mahiri, mchapakazi na mtumishi wa wananchi aliyeweka maslahi ya taifa mbele.
Aidha, amesema kuwa Mkoa utaendelea kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Peramiho na taifa kwa ujumla.
Vilevile, amesema kuwa kufuatia msiba huo, viongozi mbalimbali wa Serikali watahudhuria, akiwemo Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi; Waziri Mkuu, Mwigulu Lameck Nchemba; na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: