Ni nani Aliyetenda Dhambi? | Who Sinned? [18.09.2025] Kuhani James
Автор: Kuhani James
Загружено: 2025-11-05
Просмотров: 39
Yohane 9:1-12 BHN
[1] Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu mmoja, kipofu tangu kuzaliwa.
[2] Basi, wanafunzi wakamwuliza, “Mwalimu! Ni nani aliyetenda dhambi: Mtu huyu, ama wazazi wake, hata akazaliwa kipofu?”
[3] Yesu akajibu, “Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake.
[4] Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
[5] Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu.”
[6] Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
[7] akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Hapo, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
[8] Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?”
[9] Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!
” [10] Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?”
[11] Naye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: ‘Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.’ Hapo, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.”
[12] Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Naye akawajibu, “Mimi sijui!”
#somo #live #kuhanijames mzeewayesu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: