HISTORIA YA WARANGI NA IRANGI YAO
Автор: Zara Africa
Загружено: 2025-11-15
Просмотров: 11964
WARANGI
Wamasai wanawaita "Kimalandu" waswahili wanawaita "Warangi" lakini wao hujiita "Valangi'
Kabila hili ni miongoni mwa makabila yaliyoingia nchini Tanzania yakitokea kaskazini. Kupitia "Mjikenda" kwa sasa "Kenya"
Kituo cha awali cha Warangi ni "milima ya Irangi" hasa katika kijiji cha Haubi. Historia inaonesha kuwa Warangi walianza kutawanyika wakitokea hapo.
IRANGI.
Hili ni eneo ambalo ni makazi ya kabila la warangi. Eneo hili limegawanyika ktk sehemu kuu mbili
Sehemu ya Kwanza ni Ukanda wa safu za milima inayoanzia Kondoa mjini kuelekea kaskazini hadi Bonga karibu na mji wa Babati mkoani Manyara.
HILI eneo huitwa irangi ya juu. Safu hizi za Milima huitwa milima Kolo.
Sehemu ya Pili ni ni tambarare ya mashariki inayoanzia Busi hadi wilaya ya Handeni, Kwa kaskazini bonde linaanzia Mnenia hadi Kilimanjaro. Kwa upande wa magharibi ni kuanzia bonde la mto Bubu hadI Singida. Na kusini ni kuanzia mji wa Kondoa hadi kuungana na bonde la Rufiji.
Katika safu hizi za milima Kolo kuna vilele mashuhuri katika ukanda wa Haubi vyenye baridi kali. Pia kuna Kilele cha mlima mrefu wa Ncholincholo ulioko kati ya kijiji cha Kolo na Mnenia ambako kuna nyayo za binadamu aliyekanyaga kwenye mawe ambazo bado zinaonekana mpaka sasa,
Pia kuna mlima Kaha ambao ni mlima mrefu ulio kati ya Bolisa, Hachwi na Changaa.
Katika eneo hili la milima inayozunguka kijiji cha Bolisa ndiko kuliko na michoro mingi ya mapangoni.
...............
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: