MGOMBEA ALIVYO PIGA MAGOTI NA KULIA MBELE ZA WAJUMBE AKIOMBA KURA ZA NDIYO | SAUTI YA SIMBA
Автор: IPC Mkombozi TV
Загружено: 2025-07-31
Просмотров: 50286
Mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Nguvu Chengula maarufu kama Sauti ya Simba, amepiga magoti pamoja na kutishia kulia machozi mbele ya wajumbe wa CCM Kata ya Kihesa, wakati akiomba kura ya ndiyo ili kupata ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza kwa hisia kali, Chengula alisema amekitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu kwa moyo wa dhati, nguvu zake zote, na hata fedha zake alizowahi kuwa nazo, akisisitiza kuwa amekuwa mwaminifu kwa chama licha ya kushindwa katika chaguzi zilizopita.
Amesema kuwa endapo atapewa nafasi hiyo, ataweka kipaumbele katika kuboresha sekta ya elimu, afya na miundombinu, akiahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Iringa Mjini.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: