ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI DODOMA KATIKA MAENEO MAALUM YA KIUCHUMI (NALA)
Автор: Uwekezaji TV
Загружено: 2025-09-24
Просмотров: 63
Ziara ya Waandishi wa Habari Dodoma Katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi:
TISEZA Yalenga Kuongeza Uwekezaji Nala Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imeendelea na juhudi za kuhamasisha wawekezaji kupitia ziara maalum kwa waandishi wa habari, ambapo waandishi hao walitembelea eneo la uwekezaji la Nala, lililopo jijini Dodoma.
Lengo la ziara hii lilikuwa ni kuwapa waandishi wa habari fursa ya kuona kwa macho yao hali ya eneo hilo, na kuelewa vigezo na mazingira yaliyowekwa na Serikali ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Kanda ya Kati wa TISEZA, Venance Mashiba, alisema kuwa maeneo maalum ya kiuchumi, kama Nala, yanatoa fursa kubwa za uwekezaji na ni eneo linalofika, miundombinu, umeme na maji tayati vipo katika eneo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: