MRADI WA MATANGI YA KUHIFADHI MAFUTA UTAKAVYOIPAISHA TANZANIA KIUCHUMI. PROF. MBARAWA AELEZA
Автор: ufmradiotz
Загружено: 2025-11-27
Просмотров: 84
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amekagua maendeleo ya ujenzi wa matangi 15 ya kuhifadhia mafuta yanayotekelezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa gharama ya Sh bilioni 703 katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam.
Mradi huo ulioanza Agosti 2024 unatarajiwa kukamilika Agosti 2026 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 33.57 na ujenzi wa misingi na nguzo muhimu za matenki ukiwa umekamilika.
Profesa Mbarawa amesema matanki hayo yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 378,000 na yatapunguza foleni za meli za mafuta pamoja na gharama za uingizaji.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Dk. Baraka Mdima, alisema kazi inaendelea kwa kasi na maandalizi ya msingi wa matenki yamekamilika, huku awamu nyingine zikiendelea kama ilivyopangwa.
Mhariri | @rajjmsangi
#UFMUpdates
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: