UTAPENDA HII NGOMA YA WAYEYE YENYE MAJOKA YA KUTISHA….NYANGUKU WAMEFURAHI.
Автор: MwangazaTV
Загружено: 2025-10-15
Просмотров: 94
#mwangazatvupdates
Wakazi wa kata ya Nyanguku wamepata burudani ya kipekee baada ya kikundi cha wachezaji wa ngoma za asili, Wayeye, kutumbuiza kwa mbwembwe katika moja ya kampeni. Onyesho hilo lilijaa shamrashamra, huku Wayeye wakivutia umati mkubwa kwa mitindo yao ya kucheza ngoma wakishirikiana na majoka ya kutisha.
Majoka hayo, yaliyotengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu na kupambwa kwa rangi ang’avu, yaliingia kwa kishindo na kuongeza mvuto mkubwa kwenye tukio hilo. Uchezaji wao wa kuvutia uliwachanganya watazamaji, wengine wakicheka kwa furaha huku wengine wakijificha kwa uoga wa burudani.
Onyesho hilo lililovutia watu wa rika zote, liliwacha wengi wakishangilia na kupongeza kipaji cha Wayeye. Wakazi walieleza kuwa wamefurahia sana burudani hiyo, wakisema haijawahi kushuhudiwa kwa muda mrefu katika eneo hilo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: