MBUNGE JOHN NZILANYINGI AMKABILI MKANDARASI, ATAKA KASI YA UJENZI WA DARAJA LA MKUYUNI IONGEZEKE.
Автор: Jambo FM Radio Tanzania
Загружено: 2025-12-05
Просмотров: 14
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Nzilanyingi, amemtaka mkandarasi anayejenga Daraja la Mkuyuni kukamilisha mradi huo ifikapo Januari 28, 2026, ili kuondoa adha wanayoipata wananchi na watumiaji wa barabara hiyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Nzilanyingi amesema ujenzi wa daraja hilo umekuwa kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo, na kwamba ataendelea kufuatilia kwa ukaribu hatua za ujenzi hadi mradi ukamilike.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza walioambatana na mbunge huyo wamemuomba mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuwa mradi huo umekuwa ukisuasua na uko nje ya makubaliano ya awali ambapo wamesema daraja hilo lilipaswa kuanza kupitika mwishoni mwa Novemba 2025, lakini hadi sasa ujenzi haujakamilika.
Kwa upande wake, Ipimilo Dwasi, Mhandisi wa Madaraja kutoka kampuni ya Jasco Co. Ltd, amesema ucheleweshwaji wa baadhi ya mabomba ya maji yaliyopaswa kuondolewa katika eneo la mradi ndiyo sababu kuu iliyochangia kazi kusimama kwa muda.
Daraja hilo lenye upana wa mita 15 na njia sita lilianza kujengwa Novemba 13, 2024 na lilitakiwa kukamilika Novemba 13, 2025, lakini hadi sasa kazi inaendelea.
#jambofmtanzania #news #chaguamaishafresh
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: