Simulizi wachimbaji wawili waliofukiwa siku 9 mgodini, waokolewa wakiwa hai
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-08-13
Просмотров: 987
Wachimbaji wadogo wawili Mpina Shukuru (29) mkazi wa Mganza, wilayani Chato na Renatus Nyanga (35), mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza, wameokolewa wakiwa hai, baada ya kufukiwa na kifusi siku tisa, katika mgodi wa Igalula; wilayani Nyangwale, Mkoa wa Geita.
Wachimbaji hao walifukiwa na kifusi usiku wa Agosti mosi, 2023; wameokolewa Agosti 11 huku wakiwa wamedhoofika na kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari waliokuwa eneo la tukio, kisha kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale kwa matibabu zaidi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: