Elimu Yatolewa Kudhibiti Ubakaji, Usagaji, Ulawiti Wanafunzi Ukerewe
Автор: Ukerewe District Council
Загружено: 2025-02-21
Просмотров: 241
Elimu Yatolewa Kudhibiti Ubakaji, Usagaji, Ulawiti Wanafunzi Ukerewe
Na: Dotto Manumbu, Ukerewe
Zaidi ya Wanafunzi 2000 wamepatiwa elimu ya kujikinga na matendo ya ubakaji, ulawiti, usagaji pamoja na mimba za utotoni hali ambayo hupelekea kuzima ndoto zao.
Elimu hiyo imetolewa leo Februari 21, 2024 katika Shule ya Msingi Ihebo na Shule ya Sekondari Chief Lukumbuzya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya elimu ya msaada wa kisheria ya Mama Samia "Mama Samia Legal Aid Campaign" ambayo imegusa imegusa changamoto za wanafunzi na kuzitatua.
Awali, akitoa elimu hiyo, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Vick Mbunde amewaelekeza wanafunzi kutoshirikikutoshiriki masomo yao vizuri na kujiepusha masuala ya kubeba mimba katika umri mdogo.
"Usije Shule ukaja kubeba mimba, tunakataza wanafunzi wote kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo, na pia ni marufuku mwanafunzi kushiriki mapenzi ya jinsia moja, ni kosa kisheria, tujibidishe katika elimu" Alisema Mbunde
Mbunde amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewatua mzigo wazazi kwa kutoa elimu ya msingi na sekondari bure, hivyo amewasisitiza wazazi kuandikisha watoto wote waliotimiza umri wa kuanza masomo ya elimu ya msingi na sekondari.
"Kila mwanafunzi anahaki ya kupata elimu iliyo bora, ndio maana serikali kupitia Sera zake mbalimbali na sheria tumeweka elimu bure, kila mtoto anaefikisha umri wa miaka mitano aanze kupata elimu, ni jukumu la kila mzazi anasimamia maelekezo hayo ya serikali" Alisisitiza
Kwa upande wake msajili msaidizi wa mashirika yasiyo ya serikali wilayani Ukerewe mkoani Mwanza Bi. Rhoda Ogada akiwa katika Shule ya Msingi Ihebo amewaasa wanafunzi kutoa taarifa katika mamlaka husika pale wanapoona masuala ya ubakaji, ulawiti, usagaji na wizi ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wahusika.
"Wewe kama mtoto wa kike ukibakwa usinyamaze, toa taarifa kwa walimu wako ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika, pia tutambue kuwa kuna madhara ya kubakwa ikiwepo kupata magonjwa ya Ngono na kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi hali ambayo husababisha hasara kubwa ya kuyaharibu maisha yako" Alisema Oganda
Pamoja na utoaji elimu hiyo, Oganda alipata fulsa ya kuzungumza na wanafunzi faragha kwa wenye changamoto mbalimbali wanazopitia katika makazi yao na kwa kushirikiana na timu nzima ya "Mama Samia Legal Aid Campaign" walifanikiwa kutoa ushauri na kutatua baadhi ya changamoto zilizowasilishwa.
Nae Mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza Koplo. Bernadetha Daudi amewaagiza wanafunzi kushiriki katika kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili hatua zichukuliwe kwa uharaka.
"Hatuwezi kufumbia macho matukio ya aina hii, sisi kama dawati la jinsia na watoto wilayani hapa tupo tayari kuhakikisha tunapambana na wale wote wanavunja sheria zetu, lengo kuu ni kulinda utu wa mtu, kujenga jamii imara, kuendeleza tabia njema kwa watoto pamoja na kuandaa vijana wenye nguvu, hekima na hofu ya Mungu ambao wataliletea maendeleo Taifa lao" Alisema Daudi
Akipongeza juhudi za Mheshimiwa Rais wa Tanzania katika kubuni na kutekelezwa kwa kampeni hiyo, Furaha Manyama (13) Mwanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ihebo amesema elimu waliyoipata imesaidia kukuza uelewa kwa kutambua madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia.
"Sisi wanafunzi wa Ihebo Shule ya Msingi, kwa niaba ya wanafunzi wote wa kike, tunampongeza Mhe Rais Samia kwa kutuletea elimu hii, baadhi ya watu walionekana kunyanyasika, kuonewa kwa kubakwa na kukosa njia za utatuzi, hivyo kwa elimu hii, tunamuahidi Mhe Rais, tutakuwa mabarozi kwa kuwapatia elimu hii vijana na watu wengine katika jamii" Alisema Manyama
Aidha, Mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule hiyo Michael Mulungu ametoa pongezi kwa serikali kwa kutenga muda na gharama katika kuwafikishia elimu hii, hali ambayo amesema imewafanya kutambua haki zao kama watoto, sheria na njia za kuwasilisha malalamiko na taarifa zinazohusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
"Tumeshauliwa sisi vijana tujiepushe na masuala ya wizi, usagaji, ubakaji na matukio yote yanayojihusisha na ukatili wa kijinsia yanayotokea katika jamii yetu ili yachukuliwe hatua za utatuzi, pia tutashirikiana na serikali kuhakikisha tunatoa taarifa za matukio kama haya ili wahusika wachukuliwe hatua" Alisema Mulungu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: