UJUMBE WA BIKRA MARIA KWA SISTER AGNES WA AKITA HUKO JAPANI MWAKA 1973
Автор: Mawaridi Media
Загружено: 2024-10-03
Просмотров: 136
SIMULIZI NA UJUMBE WA BIKIRA MARIA ALIPOTOKEA JAPANI MWAKA 1973
Anaandika Beatus Benedicto Mushumbusi
Lazima kutubu dhambi na kurekebisha maisha
Kijiji cha Akita, Japan, 1973
Ujumbe :
"Kama watu hawawezi kutubu dhambi na kurekebisha maisha yao, Baba ataupa ubinadamu adhabu kali sana. Itakuwa adhabu kali zaidi kuliko gharika ya wakati wa Nuhu ambayo hakuna mtu aliyewahi kuiona."
(Bikira Maria kwa Sr. Agnes, Oktoba 13, 1973).
Tarehe 22 Aprili, 1984, baada ya miaka minane ya uchunguzi, na baada ya mawasiliano na Vatikani, ujumbe wa Mama yetu wa Akita ulithibitishwa na Askofu wa Jimbo.
Katika kijiji cha Akita, sanamu ya Bikira Maria, kadiri ya uthibitisho wa watu wapatao 500 wakristo na wasio wakristo, akiwemo meya wa mji huo wa dini ya Buddha, ilianza kutoa jasho, damu na machozi. Mtawa mmoja, Sr. Agnes Katsuka Sasagawa, amepokea ujumbe kutoka kwa Bikira Maria.
Matukio yasiyo ya kawaida yalianza tarehe 12 Januari, 1973, wakati Sr. Agnes alipoona mionzi mikali ya ajabu ya mwanga ikitoka kwenye tabenakulo. Matukio hayo hayo yalitokea siku mbili zilizofuata.
Tarehe 28 Juni, 1973, kidonda kilichokuwa na umbo la msalaba kilitokea katika mkono wa Sr. Agnes, upande wa ndani. Kidonda hicho kilikuwa kinatoka damu sana na kumfanya apate maumivu makali sana.
Tarehe 6 Julai, 1973, Sr. Agnes alisikia sauti ikitokea kwenye sanamu ya Bikira Maria iliyokuwemo katika kanisa ambamo alikuwa anasali. Sanamu hiyo ilitenge- nezwa kwa mti wa aina ya Katsura na ilikuwa na urefu wa futi tatu. Katika siku hiyo hiyo Masista wachache waliona matone ya damu yakitiririka kutoka mkono wa kulia wa sanamu hiyo.
Baadaye damu ikatiririka tena hata kwa mara ya tatu na ya nne. Kidonda katika mkono wa sanamu kilibaki mpaka tarehe 29 Septemba, ndipo kilipotoweka.
Miaka miwili baadaye, tarehe 4 Januari, 1975, sanamu ya Bikira Maria ilianza kulia machozi. Iliendelea kulia mara kwa mara kwa muda wa miaka 6 na miezi 8. Katika muda huo ililia mara 101.
Mwaka 1984 Askofu Ito alilitambua rasmi tukio hilo pamoja na ujumbe wa Bikira Maria kwa Sr. Agnes. Tangu wakati huo mahujaji wengi walifika mahali hapo toka pande zote za dunia kuja kushuhudia. Kardinali Ratzinger alimpokea Askofu Nigata Ito wa Jimbo la Nigata, na kuamua kwamba ujumbe wa Bikira Maria ulikuwa wa kuaminika.
Ufuatao ni ujumbe wa Mama yetu wa Akita kwa Sr. Agnes:
Julai 6, 1973
"Binti yangu, umenikubali Mimi kwa kuacha yote na kunifuata. Je, udhaifu wa masikio yako unakuletea maumivu? Hali yako ya kuwa kiziwi itaponywa. Uwe na hakika juu ya jambo hili. Uwe mvumilivu. Hili ni jaribu la mwisho. Je, kidonda cha mkono wako kinakuuma? Sali kwa ajili ya malipizi ya dhambi za watu".
Agosti 3, 1973
"Binti yangu, watu wengi katika dunia hii wanamkosea Mungu. Natamani roho zimfariji Yeye na kupunguza hasira yake Baba yetu aliye mbinguni. Natamani, pamoja na Mwanangu, roho ambazo zitajirekebisha kutokana na mateso na umaskini kwa ajili ya wenye dhambi."
Oktoba 13, 1973
"Binti yangu, sikiliza kwa makini yale yote nitakayokuambia: Kama nilivyokuambia kwamba ikiwa watu hawawezi kutubu na kujirekebisha wao wenyewe, Baba atawaletea adhabu kali. Itakuwa adhabu kubwa zaidi kuliko gharika ambayo haijawahi kutokea. Moto utaa- nguka chini kutoka mbinguni na kufutilia mbali sehemu kubwa ya wanadamu, wema na wabaya, bila kubakiza mapadre na wengine wote washika dini. Watakaosalimika watajikuta katika hali ya upweke na kwamba watawaonea wivu wale wote waliokufa. Silaha ya pekee itakayobaki kwenu ni Rozari na Alama iliyoachwa na Mwanangu. Kila siku mtasali Rozari. Kwa njia ya Rozari, salini kwa ajili ya Papa, Maaskofu na Mapadre."
#Mawaridimedia
#catholicchurch
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: