#MBULU
Автор: Come Tv Tanzania
Загружено: 2024-04-22
Просмотров: 174
COME TV NEW: MBULU YAFANYA MAOMBI YA KUOMBEA TAIFA KUELEKEA MIAKA 60 YA MUUNGANO, MGENI RASMI NI MKUU WA WILAYA YA MBULU MHE.VERONICA KESSY
🗓️ 22-04-2023
📍 UWANJA WA MBULU MJI
Mapema hii leo COME TV ilipata nafasi ya kuhudhuria maombi ya kuliombea Taifa na kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
mgeni rasmi ni alikuwa mkuu wa wilaya mbulu Mhe.VERONICA KESSI Maombi hayo ya mefanyika katika uwanja wa Mpira wa Miguu Mbulu Mji.
viongozi mbalimbali wa Dini waliweza kuhudhuria ambao ni wachungaji, shekha, pandre na kiongonzi wa mila.
Aidha mhe.Veronica Kessy amempongeza rais kwaajili ya kufanya kumbukizi ya muungano ambao unatimiza miaka 60 amesema "taifa letu ni taifa ambalo linaonewa wivu na mataifa mengin ya nje kwa sababu ya mshikamano tulionayo, Mshikamano ambao sasa unafikisha miaka 60."
Kauli mbiu ya muungano ni "MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA TUMESHIKAMANA, TUMEIMARIKA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU".
Mhe.Veronica Kessy Mkuu wa Wilaya ya Mbulu amewaasa wananchi wa wilaya ya Mbulu kuwa katika jambo lolote tumtangulize mungu, Hivyo tunapokuwa na tukio kama hili la kuliombea taifa, hatuna budi wananchi wote kujitokeza.
Mfanyakazi wa wilaya ya mbulu Ndg.Frank Rwechungura amesema tukio lolote huanza na Imani, Maandali, na maadili huanza kwenye suala la dini amesema tukio hilo ni la muhimu na la kipekee katika jamii.
Pia ametoa ushauri wake kwa kusema iwe ni maendelezo kwa sababu unapotaka kujenga kiongozi bora au jamii ni lazima uanze na msingi ya imani, na msingi ya imani inapatikana katika dini iwe ya kiislamu, au kikristo kwa sababu hakuna dini inayomfundisha mtu kuiba.
Pia Ndg Philbert Lugaimukamu Ambaye ni Afisa elimu kata ya Endagikot amesema maombi haya ya dua ya kuenzi miaka 60 ya muugano ni kitu kinzuri kwa halmashauri ya wilaya mbulu. Amese kwamba amefarijika na maombi haya kwa sababu ushikiano ulioneshwa na viongozi mbalimbali wa dini. Ambao ni shekha, pandre, wachungaji na kiongozi wa mila.
Ameshauri kwa kusema miaka ijayo maandalizi yafanyike mapema ili waonyeshe mwitikio mkubwa zaidi.
#Kwa pamoja tunaijenga Mbulu yetu.
#Kazi iendelee
Mwandishi: Daniel Mayko
Powered by Come tv Tz online
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: