Jengo la Kituo Kikuu cha Polisi kuondolewa kupisha upanuzi wa Bandari ya Mwanza
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-03-16
Просмотров: 1396
Cheza sasa kupitia https://shorturl.at/jqzU6 na ushinde
Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
Kamati ya Kudumu ya Bunge Miundombinu imeagiza kuondolewa jengo la Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Mwanza na wafanyabiashara wanaouza samaki eneo la Kamanga kupisha upanuzi wa gati la Bandari ya Mwanza Kaskazini jijini humo.
Maagizo hayo yametolewa leo Jumamosi Machi 16, 2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Selemani Kakoso, wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa upanuzi wa bandari hiyo unaogharimu Sh18.6 bilioni.
Kakoso amemwagiza Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni ili kujadiliana na kupata mwafaka wa kuondolewa jengo hilo, huku akiwataka wauzaji wa samaki soko la Kamanga kupisha eneo hilo kwa hiari ili kuruhusu utekelezaji wa mradi huo.
“Kwenye maeneo ambayo ni milki za Serikali wananchi kama wanayatumia ndivyo sivyo, wapishe ili mradi uweze kuendelea kufanya kazi. Mradi huu (upanuzi wa bandari) ni wa kimkakati, ambao Serikali imewekeza fedha nyingi. Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga reli inayokuja hadi hapa bandarini na meli.
“Maeneo yote ambayo wanatakiwa kupisha ni pamoja na eneo la Jeshi la Polisi na kwa kuwa Jeshi la Polisi na bandari ni mali ya Serikali, Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa Mambo ya Ndani watakaa ili kuhakikisha maeneo haya wanapisha ili mradi wa upanuzi wa bandari uweze kufanya kazi vizuri,” amesema Kakoso.
Awali, Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Erasto Lugenge amesema utekelezaji wa mradi huo ulioanza Mei 3, 2023, kwa mkataba wa miezi 18 umefikia asilimia 30 ukijumuisha ujenzi wa maegesho, barabara ya sakafu ngumu, jengo la abiria na ujenzi wa uzio wa bandari hiyo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: