Kanisa la Methodist Tanzania latoa msimamo wake maziko ya Askofu aliyedaiwa kujinyonga
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-05-19
Просмотров: 8761
Wakati mwili wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania (TMC), Joseph Bundala ukitarajiwa kuzikwa kesho Ihumwa jijini Dodoma, Makamu wa askofu wa kanisa hilo, Samweli Nyenza amesema msimamo wa kanisa hilo ni kwamba mtu aliyeua au kujiua mwenyewe ametenda dhambi.
Askofu Nyenza ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Mei 19, 2024 wakati akizungumza na Mwananchi Digital eneo la Ihumwa, nyumbani kwa marehemu Bundala, ambaye alikutwa amekufa akidaiwa kujinyonga ofisini kwake, kwenye kanisa hilo, Ipagala jijini Dodoma.
Askofu Nyenza amesema kuua au kujiua ni dhambi, hivyo hawaungi mkono vitendo hivyo na hata ikibainika kiongozi wa ngazi ya juu wa kanisa hilo au muumini wa kawaida amefanya kitendo hicho hawatamuunga mkono.
Kuhusu maziko ya askofu Bundala kama atazikwa kwa heshima au hatazikwa kwa heshima kutokana na kujiua, askofu huyo amesema kuwa wanasubiri ripoti ya Polisi kujua ukweli wa tukio hilo, ndipo wajue kama watamzika kwa heshima zote au la.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: