SHEREHE YA MAHAFALI YA 15 DARASA LA 7, MAPS ( MBEYA ADVENTIST PRE & PRIMARY SCHOOL)
Автор: Hope Media SHC
Загружено: 2025-08-22
Просмотров: 223
MBEYA
Wito umetolewa kwa Wazazi na walezi kuendelea kulinda viwango vya malezi walivyo navyo watoto wanapokuwa nyumbani mara baada ya kuhitimu masomo yao
Wito huo umetolewa na Mhandisi Yusuphu Bigurube ambaye amehudumu kama mgeni rasmi katika sherehe za mahafali ya 15 ya darasa la saba katika shule ya Maps Mbeya na kusema kuwa wazazi wana jukumu la kuhakikisha wanalinda uwezo na maendeleo ya watoto wawapo uraiani
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa shule ya Maps Brown Bukuku pamoja na mkurugenzi wa elimu Mch. Meshack Zilakwega wamesema utekelezaji wa sera ya elimu ya kiadventista umewasaidia sana kukua na kuendelea katika katika Nyanja zote
Nao wazazi, walezi pamoja na wanafunzi wakiongea katika mahafali ayo wamesema elimu inayotolewa shuleni hapo imekuwa na mchango mkubwa sana katika kujenga malezi ya watoto kiroho na kijamii
Hii ni mahafali ya 15 kwa shule hii ya awali na Msingi Maps inayopatikana jijini Mbeya ambapo takribani wanafunzi 89 wamehitimu masomo yao ya darsa la saba tayari kwa hatua nyingine ya kimasomo
Na George Muttarogwa
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: