STAR TV - MAISHA YA OLOIBONI MESHUKO OLE MAPII
Автор: Raymond Nyamwihula
Загружено: 2013-01-11
Просмотров: 305544
Mzee Mapii ni Mmoja wa Viongozi wa mila (Oloiboni/Laiboni) wa Jamii ya Wafugaji ya Wamaasai ambaye anajaribu kuonyesha mfumo tofauti wa kimaisha akiwa anajiendeleza pamoja na Familia yake kwa kutumia rasilimali mifugo aliyonayo.
Oloiboni Mapii amemudu kuweka mfumo wa Umeme wa Jua katika Boma lake na akijenga Majiko sanifu kukabiliana na adha za kiafya kwa Wake zake, Watoto, Wajukuu na Vitukuu.
Licha ya kutopata bahati ya kwenda Shule lakini amehamasika kujenga Shule ya Msingi iliyo jirani na Makazi yake; Shule hiyo wakisoma Wajukuu na Vitukuu vyake pamoja na Watoto wengine jirani na Boma lake. Kilio chake ni Walimu katika Shule yake pamoja na Makazi ya Walimu hao.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: