MBUNGE WA MBEYA VIJIJINI ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MVUA
Автор: BONGO PLAY TELEVISION
Загружено: 2026-01-24
Просмотров: 6
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida, ametembelea wananchi waliokumbwa na madhara ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wa Mbeya.
Ziara hiyo imelenga kujionea hali halisi ya uharibifu uliosababishwa na mvua hizo pamoja na kuwapa pole waathirika.
Katika maelezo yake, Mbunge Patali amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika upandaji miti kama njia ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kupunguza athari za majanga ya asili. Mvua hizo zimesababisha kuharibika kwa Shule ya Sekondari Usongwe pamoja na makazi ya zaidi ya familia tano.
Kwa upande wao baadhi Wananchi wameeleza kwa kina namna walivyokumbwa na tukio hilo na kumpongeza Mbunge kwa kufika eneo la tukio na kuonyesha mshikamano.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: