Azam FC yasema ipo tayari kuivaa Simba SC
Автор: Azam TV
Загружено: 2025-12-06
Просмотров: 379
Mzizima DERBY: “Timu mbili kubwa zitakuwa tayari kwa mechi hii”
Kocha msaidizi wa Azam FC Addis Worku, anasema kesho Jumapili zinakutana timu kubwa na amewaita mashabiki kwenda kuitazama mechi hiyo na wale watakaoshindwa, watazame kwenye kisimbuzi cha #AzamTV.
Kocha huyo anasema swala la kupoteza nafasi halikwepeki kwenye soka, lakini jambo la muhimu ni kutengeneza nafasi.
Worku anasema muhimu kwao ni kutengeneza nafasi zaidi kuliko kuruhusu magoli na kadri muda uanavyokwenda, watakuwa wanashinda zaidi kuliko kutoa droo.
Kwa upande wake mshambualiaji Nassor Saaduni anasema wamekuwa wakihamasishana na wapo tayari kuikabili Simba.
#MzizimaDerby #SimbaVsAzamFC #SimbaSC #AzamFC
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: