🌐VIJANA MTWARA WATAKA FURSA SIYO MAANDAMANO
Автор: KITAMA UPDATE ONLINE TV
Загружено: 2025-12-02
Просмотров: 201
Vijana wa mkoa wa Mtwara wamesema wanahitaji Serikali iwasaidie kuwajengea mazingira wezeshi ili wanufaike na fursa za kiuchumi zilizopo ikiwemo kuzalisha ajira na kudumisha amani kwa lengo la kukuza maendeleo ya Taifa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na vijana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana na mbunge wa Mtwara Mjini Joel Nanauka leo (29 Novemba 2025) amesema Serikali itatumia muda mwingi kutafuta fursa za maendeleo kwa vijana badala ya kudhibiti vijana.
Aidha, Waziri Nanauka aliwaeleza vijana kuwa dhmaira ya kuundwa wizara maalumu ya maendeleo ya vijana ni kutekeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona mawazo na fikra za vijana nchini zinasikika ili kutatua changamoto zao.
Mhe. Nanauka aliongeza kusema katika kuhakikisha vijana wanapata mitaji na kuwa na uhakika wa kipato amekusidia kuanzisha mfuko maalum wa vijana (Saccos) waendesha pikipiki na akina mama wajasiliamali ambapo atachangia mfuko uwe na uwezo wa kukopesha vijana itakayowasaidia kuwa na uhakika wa ajira.Nanauka amewataka vijana wa mkoa wa Mtwara kuitunza amani na kwamba kama alivyoahidi wakati wa uchaguzi, ataendelea kuwa mtumishi wa wote kwa maendeleo ya wote ambapo amewataka vijana wenye mawazo ya ubunifu wa biashara kuwasiliana na ofisi yake ili utaratibu wa kuwasaidia kuboresha mawazo hayo kuwa biashara ufanyike.
Vijana wakizungumza kwenye ziara hiyo akiwemo Hamza Kalinga mkazi wa kijiwe cha kahawa cha Chilindima alisema vijana wa Mtwara hawahijati maandamano kwa kuwa hata baaada ya uchuguzi mkuu uliopita hawakushiriki kwenye vurugu badala yake mahitaji kusikilizwa na kupatiwa fursa ikiwemo mitaji ya kuanzisha biashara.
Waziri Nanauka yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya kukutana na vijana na kusikiliza maoni na mawazo yao kuhusu Tanzania wataitakayo ambapo leo ametembelea mtaa wa Mdenga, Muungano, Chilindima, stendi ya Mkanaledi na stendi ya Mikindani akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Kedmon Mapama pamoja na viongozi wa Mkoa huo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: