MATARAJIO YASIYO SAHIHI: PASTOR BARAKA TEGGE; 25.06.2020
Автор: Josephat Gwajima RudishaTv
Загружено: 2020-06-25
Просмотров: 1928
MATARAJIO YASIYO SAHIHI
Matarajio ni mambo ambayo mtu anategemea kuhusu jambo fulani. Matarajio yote ambayo sio sahihi ni yale ambayo unayatarajia lakini hayatakuja yatokee.
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
MIT. 13:12 SUV
Watu wengi wana mtazamo usio sahihi kuhusu maisha; watu wengi kuna mambo wanayoamini ndio maisha ingawa mambo hayo sio sahihi.
Utoshelevu wa kweli hauletwi na vitu unavyotarajia kupata au unavyotazamia kupata.
Moyo ukiharibika maisha yameharibika.
Mafanikio kwenye maisha ni kulitumikia kusudi la Mungu kwenye maisha yako.
Kupoteza nafsi kwenye Biblia ni kupoteza maisha ambayo Mungu alikuumba uyaishi.
Jambo la muhimu kuliko yote duniani ni kuujenga ufalme wake.
Mojawapo ya taabu zetu tulizonazo ni vitu tivyonavyo ambavyo hatuviitaji kwenye kutimiza kusudi la Mungu kwenye maisha yetu
Kuna kitu hukiitaji na hicho Mungu hana mpango wa kukupatia; ikitokea ukakikosa moyo unaumia,ukikipata kinaharibu moyo.
Chochote unachopata kwa juhudi zako bila Mungu kitakuumiza wewe na uzao wako. Ugomvi wa middle east ni matokeo ya baba mwenye nyumba Ibrahimu aliyezaa na housegirl.
Umri sahihi wa kuweka vipaumbele sahihi vya maisha ni umri wa ujana.
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake
MT. 6:25-34 SU
Training is more powerful than teaching; training ni kazi ya baba na teaching ni kazi ya mama.
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
LK. 4:16 SUV
Desturi ya Yesu kwenda hekaluni aliipata kwa wazazi wake.
Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; LK. 2:41-42 SUV
DUNIANI ULIKUJA KULITUMIKIA KUSUDI LA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: