PPRA, VETA zaingia makubaliano ya kuibua na kusajili vikundi maalum
Автор: The Chanzo
Загружено: 2025-11-20
Просмотров: 141
Dodoma: Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi VETA zimetia saini hati ya mkataba wa makubaliano wa kuibua na kusajili makundi maalum, lengo likiwa ni kutoa fursa za tenda za Serikali zilizotengwa kwa ajili ya makundi hayo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Denis Simba amesema, mpaka sasa jumla ya vikundi takriban 1000 vimejisajili kwenye mfumo wa NeST.
“Sheria yetu inatuelekeza iwe ni kundi kati ya watu watano mpaka watu 20. Na hapo, tumekimbia marathon miezi michache iliyopita mwaka jana nakumbuka tulikuwa na makundi 185, pamoja na kufanya kampeni nchi nzima. Lakini baada ya kuongeza kasi leo tumeona tumeongezeka kwa zaidi ya asilimia 700, 800,” amesema Mkurugenzi huyo Novemba 20, 2025 mkoani Dodoma.
“Na kwa maana hiyo vimeweza kuomba zabauni, na mikataba yenye thamani ya takriban bilioni 30 imeshatolewa kwa makundi maalum. Sasa mnaona hii gepu kubwa, tukitekeleza wote tutafikia trilioni tano [5]. Tunahitaji kuongeza kasi, ya kuwafikia wananchi.”
The goal is to increase the participation of special groups in Government tender opportunities.
You can follow us via;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Or visit our website: https://www.thechanzo.com
Do you have news? contact us via Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: