KIGOGO WA ACT WAZALENDO APINGA MPINA KUGOMBEA URAIS, ADAI KANUNI ZIMEKIUKWA “SITUMIKI NA YEYOTE”
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-08-16
Просмотров: 12210
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Katibu Mwenezi wa ACT Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Naibu Waziri Kivuli wa Sanaa, Utamaduni na Michezo katika Baraza Kivuli la Mawaziri la ACT Wazalendo, Monalisa Ndala amepinga uamuzi wa Chama hicho, kumteua Luhaga Mpina kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, akidai amekosa sifa kwakuwa kanuni za Chama hicho zimekiukwa wakati wa mchakato wa kumteua.
Monalisa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu August 14,2025 akimtaarifu kwamba Mpina hajakidhi kanuni za kudumu za uendeshaji wa hicho, toleo la mwaka 2015 akisema vipengele kadhaa vya kanuni namba 16 inayozungumzia sifa za Mgombea ndani ya Chama na wanaoomba kuteuliwa kugombea ACT Wazalendo, vimekiukwa.
Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amemtafuta Monalisa kwa njia ya simu ambapo amethibitisha kuwa ni kweli ameandika barua hiyo kwa Katibu Mkuu lakini haijajibiwa na kwamba ameamua kuisambaza mtandaoni ili kuomba nguvu ya Umma isaidie kushinikiza barua yake kujibiwa huku akisisitiza kuwa hana chuki binafsi na Mpina na wala hatumiki na Mtu au Kikundi chochote kufanya hivyo bali amechukua hatua hiyo kukinusuru Chama kisipoteze Mgombea kwa kukosa sifa.
Monalisa amesema ‘Kanuni namba 16 (4) Mgombea urais / Viongozi wa ACT ngazi ya Taifa, lazima awe Mwanachama wa ACT Wazalendo kwa muda usiopungua mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya uteuzi ya Mgombea wa Chama, Mgombea wetu aliyejiunga siku mbili kabla ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais baada ya kuenguliwa kuwania ubunge kwa chama chake cha zamani (CCM) July 28, 2025”
Monalisa pia amesema Mpina amepingana na kanuni namba16 (4) (iii) inayosema awe tayari kutangaza mali binafsi na vyanzo binafsi kabla ya kuteuliwa kugombea kwa kufuata utaratibu ulioanishwa sehemu ya (vii) ya nyongeza ya Katiba ya ACT Wazalendo na kusema amevunja kanuni hii kwa kuwa hadi anatangazwa kuteuliwa kuwa Mgombea, hakuna pahala popote ameonesha kutangaza mali zake, Mpina amekiuka pia kanuni muhimu namba 16 (4) (iv)inayomuhitaji kuelewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo kama inayosomea ‘awe ni mtu aliyethibitika kuielewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo na aonyeshe utayari wa kuisimamia na kuuishi”
@AyoTV_ imefanya jitihada za kumtafuta Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu bila mafanikio ambapo juhudi za kumpata ili kupata kauli yake zinaendelea.
#MillardAyoUPDATES
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: