MBALI KULE NASIKIA | Angels we have heard on high — A Christmas song — Swahili version
Автор: Swahili Worship Hymns
Загружено: 2025-12-25
Просмотров: 17214
Mbali kule nasikia
malaika wa mbinguni,
Wakiimba wengi pia
wimbo huo juu angani:
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.
Wachunga tuambieni
sababu ya nyimbo hizo?
Mwenye kuimbiwa ni nani,
juu ya nani sifa hizo?
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.
Je hamjui jambo kuu
la kuzaliwa Mwokozi?
Habari ya wimbo huo,
Ndiyo kumshukuru Mwenyezi.
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.
Kweli, nasi twende hima,
tufike kule aliko,
Tuone mtoto na mama,
tuwasalimie huko.
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: