UZINDUZI WA GARI JIPYA LA SHULE YA TAPS TUKUYU
Автор: Hope Media SHC
Загружено: 2025-08-20
Просмотров: 170
MBEYA
Mwenyekiti wa Konferensi ya nyanda za juu kusini ametoa rai kwa washiriki na jamiii kwa ujumla kuunga mkono juhudi za maendeleo ya elimu kwa kuwapeleka wanafunzi katika shule za kanisa ili wapate maadili mema na elimu iliyo bora
Mwenyekiti wa Konferensi iyo mchungaji Toto Ndege Bwire Kusaga ametoa rai hiyo alipokuwa akifanya huduma ya uzinduzi wa Basi la shule lililo nunuliwa mahususi kwa ajili ya kutatua changamoto ya usafiri kwa wanafunzi iliyokuwa inakwamisha maendeleo ya shule kwa namna tofauti
Naye mhazini wa konferensi ya nyanda za juu kusini CPA Emanuel Chaula ambaye pia ni msimamizi wa mali za kanisa amewashukuru washiriki na wadau wote waliohusika kufanikisha upatikanaji wa gari ilo na kuwasihi kuendelea kutegemeza matukio mipango yote ya utume
Aidha mwenyekiti wa bodi ya shule Mhandisi Joseph mkeni pamoja na mkuu wa shule iyo Seth Kuyenga wamesema wanafurahishwa na hatua hiyo waliyofikia na kwamba wataendeleza jitihada za kuongeza gari nyingi Zaidi na kuongeza idadi ya wanafunzi
Kufuatia hatua hiyo wazazi na wanafunzi waliohudhuria tukio ilo la uzinduzi wa gari ya shule wameupongeza mpango huo uliowekwa mahsusi kwa ajili ya kutatua changamoto ya usafiri shuleni apo na kuwaweka wanafunza katika hali ya usalama Zaidi
Shule ya awali na msingi ya Tukuyu Adventist imeanzisha mnamo mwezi wa kwanza mwaka 2024 ikiwa imetimiza mwaka mmoja na miezi minane hivi sasa huku ikionesha ukuaji wa hali ya juu kitaaluma na kimiundombinu kwani hadi sasa ina wanafunzi 203
Na George Muttarogwa
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: