DAY 3 - NOVENA TO THE HOLY SPIRIT (NOVENA YA ROHO MTAKATIFU)
Автор: AMANI MEDIA CATHOLIC TV
Загружено: 2025-06-01
Просмотров: 34
DAY 3 | NOVENA YA ROHO MTAKATIFU| TUNAOMBA KUPATA ROHO MTAKATIFU
Welcome to Day 1 of the Novena to the Holy Spirit—the most ancient of all novenas, prayed with the Church in preparation for the great Feast of Pentecost
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU
SIKU YA KWANZA
MAKAO MAZURI YA MOYO WANGU.
Ewe Roho Mtakatifu, zawadi ya Mungu kwa moyo wangu, nina hamu kubwa na ninakutamani kila ninapofikiri kuhusu wewe. Ninakosa maneno ya kuelezea furaha ya pekee ninayoisikia ndani mwangu, nikifahamu kwamba wewe ndiwe uliye furaha ndani ya makao matakatifu ya moyo wangu. Moyo wangu umejazwa na utulivu na upendo pamoja na uchangamfu na uzuri wa tafakari yako. Ninashangazwa na namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani mwangu.
Nikifikiria uzuri wako unapita uzuri wote tunaoweza kusimulia au kufikia juu yake. Ninafikiria kuhusu utajiri wako usio na mipaka, utajiri wa neema, vipaji, fadhila, matunda na heri. Ninafikiri kuhusu uzuri wako wa pekee ambao unakuleta wewe kukaa nami daima.
Umeyashika yate, unayafanya yote, na unapenda kunipa mimi hayo yote. Ninahamu nawe na ninakutamani, pamoja na hali yangu ya maanguko ambayo inanifanya kiumbe dhaifu kuliko vyote duniani.
Ninakubariki, ninakuabudu, na ninakushukuru. Ninakuomba kila kitu. Nipe yote ewe Roho Mtakatifu.
Tuombe:
Ee Mungu uliyeijaza mioyo ya waumini wako mwanga wa Roho Mtakatifu, tupe roho yule yule ili tuweze kujua mema na tuweze kufurahi katika faraja zako kupitia kwa Kristo Bwana wetu. Amina
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: