UCHAGUZI MKUU 2025, TUNACHUKUA URAIS WA TANZANIA
Автор: Knews24
Загружено: 2025-03-30
Просмотров: 874
#knews24 Chama cha NCCR-Mageuzi kimefanya uchaguzi wake mkuu na kumchagua Evaline Munisi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo, Machi 30, 2025, katika Ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Evaline Munisi alipata kura 34, akimshinda Saganda Khalid, aliyepata kura 19 kati ya kura 53 zilizopigwa.
Wengine walioshinda ni Martin Bernad, aliyepata kura za "Ndiyo" 40, na kuchaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Shindani Ally, aliyechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar, na Suzan Masele, aliyechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa chama hicho.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Evaline Munisi, Katibu Mkuu mpya wa NCCR-Mageuzi, ameahidi kurejesha hadhi ya chama hicho kwa kuhakikisha wanashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao, huku akisisitiza kuwa hawana hofu na Chama Cha Mapinduzi (CCM). kwa sababu mabadiliko ya mfumo wa Uchaguzi yaliyokuwa yakipiganiwa tayari yalishafanyika kupitia Baraza kuu la vyama vya siasa kwa kushirikiana na Kikosi kazi kilichokuwa kimeundwa.
"Tunayo imani kubwa na mchakato wa uchaguzi kwa sababu tayari mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yameshafanyika kupitia Kikosi Kazi. Tunaiomba serikali isiruhusu watu kuvunja Katiba, kwani uchaguzi upo kwa mujibu wa Katiba, na sisi NCCR-Mageuzi tunafuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," amesema Munisi.

Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: