SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI MCHENGERWA KWA MAAFISA HABARI, DODOMA
Автор: Ukerewe District Council
Загружено: 2025-05-23
Просмотров: 144
HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHESHIMIWA MOHAMED O. MCHENGERWA (Mb) KATIKA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI WA MIKOA, MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NA TAASISI ZA OFISI YA RAIS TAMISEMI, KITAKACHOFANYIKA TAREHE 23 MEI, 2025 KATIKA UKUMBI WA JIJI LA DODOMA MJI WA SERIKALI MTUMBA MKOA WA DODOMA
Ndugu Maafisa Habari,
Kabla sijamaliza hotuba yangu nielekeze yafuatayo: -
Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa:
Hakikisheni Maafisa Habari wanashirikiki kikamilifu katika ziara zote za Viongozi pamoja na Timu za Tathimini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na uelewa wa kazi zinazofanywa na Mikoa na Halmashauri ili waweze kuzitangaza kwani Maafisa hawa ni sehemu ya timu yenu;
Kuwapatia mafunzo kazini (in service training) kama vile uandishi wa takwimu (infographics/ data Journalism), vibango, kuhariri video na mafunzo mengine kadri itakavyoonekana inafaa;
Hakikisheni Maafisa Habari wanaingia kwenye Vikao vyote vya Kisheria ili kumuwezesha kuwa na uelewa mpana wa eneo lake la Kazi kwani wao pia ni sehemu ya menejimenti kwa mujibu wa Muundo Mpya wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Hakikisheni viongozi wote wanashiriki katika vipindi vitakavyoandaliwa kwenye vyombo vya Habari vilivyopo katika maeneo yenu na vile vya Kitaifa ambavyo Maafisa Habari ndio Waratibu Wakuu wa kazi ya kujitangaza katika ngazi ya Taasisi akishirikiana na Katibu Tawala Mkoa, Mkuu wa Taasisi au Mkurugenzi wa Halmashauri;
Hakikisheni Fungu lao la Fedha (Subvote) wanapatiwa na linalipwa kwa kila mnapopata mgao (OC) au mapato ya ndani ili waweze kufanya kazi kwa weledi;
Hakikisheni mnawanunulia vitendea kazi Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri ili waweze kutimiza majukumu yao;
Hakikisheni kuwa Mikoa na Halmashauri ambazo hazina Maafisa Habari, Makatibu Tawala Mikoa fanyeni msawazo wa Maafisa Habari katika Mkoa na Halmashauri;
Hakikisheni kuwa, Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA wanafanya kazi kwa kuzingatia majukumu yao yaliyoainishwa. Mfano, Afisa TEHAMA kuhodhi nywila ya kuingilia kwenye kwenye tovuti na Mitandao ya Kijamii ya Taasisi husika; na
Hakikisheni Maafisa Habari wote wanapatiwa ofisi ili waweze kufanya kazi zao kwenye mazingira rafiki. Nimeelezwa kuwa kuna baadhi ya Maafisa Habari hawana ofisi, hivyo nawaagiza muwaelekeze Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawapatia ofisi Maafisa Habari.
Maelekezo yangu kwa Maafisa Habari:
Kila Afisa Habari aendelee kuandaa Mpango Kazi wake kutokana na Mpango Mkakati wa Taasisi/Mamlaka husika na vipaumbele vya Taasisi/Mamlaka ambavyo kwa ujumla vitasaidia Kuelimisha Umma;
Endeleeni kuwasilisha Taarifa za utendaji kazi kila baada ya miezi mitatu kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mkoa ambaye naye ataziwasilisha kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano OR-TAMISEMI kwa ajili ya kuzifanyia Tathmini na ufuatiliaji;
Hakikisheni mnakuwa wabunifu kwenye kuchakata Habari, kuziandika na kuzisambaza ili ziweze kuwafikia watu wengi;
Hakikisheni mnahuisha Tovuti na Mitandao yenu ya Kijamii kwa kuweka Taarifa za kila wakati zinazotokea kwenye maeneo yenu lengo likiwa ni kuelimisha jamii kuhusu kazi zinazotekelezwa kwenye maeneo yenu;
Hakikisheni mnaandika habari zenye hamasa na kuibua ushuhuda kuhusu kazi za Serikali na miradi inayotekelezwa ambapo Viongozi wa ngazi husika na wananchi wa kawaida wahusishwe kuusemea mradi au kazi fulani zinazotekelezwa katika maeneo yao;
Hakikisheni mnaandaa vipindi vya kutoa Elimu kwa Umma kupitia Vyombo vya Habari vya kijamii vilivyopo katika maeneo yenu na kuandaa ratiba kwa ajili ya Viongozi kushiriki kila wiki katika vipindi hivyo; na
Hakikisheni mnafuatilia taarifa za Miradi ya Maendeleo hili kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa na Taasisi zote ili kujua mradi/miradi imepata kiasi gani cha fedha halikadhalika na utekelezaji wake.
Maelekezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais TAMISEMI
Kuwasilisha Taarifa jumuishi ya Utendaji kazi wa Maafisa Habari wa Taasisi, Mikoa na Halmashauri, mafanikio na changamoto na kutoa ushauri kwa ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao ili wachukuliwe hatua za kinidhamu;
Kutumia Mkakati wa Mawasiliano unaohusisha Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
Kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii vitakavyoangazia kazi na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na virushwe kwenye Television pamoja na kutumia njia nyingine mbadala kujitangaza.
Ndugu Maafisa Habari,
Nikiendelea kuhitimisha hotuba yangu napenda niwashukuru sana ninyi Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya katika kutangaza shughuli za Serikali.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: