SASA TAYARI KWETU SIKU YA KUOKOKA
Автор: Bro. Dr. E. N.
Загружено: 2024-07-07
Просмотров: 739
SASA TAYARI KWETU SIKU YA KUOKOKA (KMC)
1. Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka,
Yesu alitimiza yote msalabani.
Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao,
Wapate kustarehe, wapone nafsi zao.
Kwa mbio:
Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana!
Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi.
Umetufanya kuwa mitume yake Mungu.
Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.
2. Wewe kwa damu yako ulikomboa sisi,
Na jua la neema linatuangazia.
Tumefahamu sasa pendo la Mungu wetu.
Damu imetuunga kati’ agano jipya.
3. Njoo upesi nawe uliyesitasita!
Mungu atakujaza neema yake kubwa,
Raha rohoni mwako inayokutuliza,
Matumaini, nguvu, pendo lililo bora.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: