RUDI UWEPONI MWAKE | MCH. KANGARAGWA KAMANZI
Автор: SAVP TV
Загружено: 2026-01-15
Просмотров: 19
MASHARIKI – SIKU YA SITA - PR KANGARAGWA KAMANZI
EZEKIEL 11:23
23 Utukufu wa Bwana ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji.
Watu wakiamua kumuacha MUNGU, yeye huwa anaamua/anachagua kuwaacha japokuwa haendi mbali nao bali anaenda nje kidogo lakini anakuwa upande wa Mashariki, ili tutakapoamua kumtafuta basi tuweze kumpata.
Upande ambao ulikuwa wa kumkimbia Bwana basi ndio upande wa kumpata Bwana kwa sababu yuko tayari kuwapokea wanaojirudi.
Uwepo wa MUNGU uliondoka/Unaondoka kwa sababu watu walimwacha au wanamwacha lakini yuko karibu sana nasi.
Ezekiel 43:1-2
Kisha akanileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki;
2 na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.
Mathayo 2:1-2
1Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Pamoja na kuwa mbali naye bado MUNGU alikufanikisha, Ukiwa mashariki upande ambao MUNGU anapatikana na akakufanikisha ni alama ya uwepo wake. Fadhili uzionazo ndizo zinaonesha uwepo wake
WITO: Amua kuja/kurudi katika Uwepo wake katika Maisha yake, toka uliko MUNGU anakusubiri uje kwake. Njoo Umsujudie, Njoo utoe Sadaka kushukuru juu ya uwepo wake maishani mwako licha ya matendo yako maovu.
Ubarikiwe unaposhiriki katika Ibada katika Jukwaa la Imo kila siku saa 11 alfajiri kupitia kiunganishi hiki.
Join us! https://s.imoim.net/j8nbAq?from=WhatsApp
Follow us on our.
Instagram account: savptv
Facebook account: savpmedia
SUBSCRIBE | COMMENT | LIKE | SHARE
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: