#LIVE
Автор: TANZANIA HABARI - TH TV
Загружено: 2025-12-29
Просмотров: 95
#ikulu #raissamia #ikuluzanzibar #uvccmtaifa #rcmwanza #rsmwanza #wazirimkuu #ccmtaifa #uvccmtaifa #uvccmmwanza #mamboyandani #mamboyanje #wizarayaujenzi #wizarayamamboyandani #wizarayaardhi
#ofisiyamakamuwarais
“MNYONGE” ALALAMIKA KUPORWA ARDHI ILEMELA
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, inatuhumiwa kupora kiwanja namba no.1840 kilichopo Buswelu “A” mali ya Matius Lubango ambacho kwa sasa imekiuza kwa mtu mwingine bila ya ridhaa ya mmiliki huyo.
Wakazi wa mtaa wa mbogamboga manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wakizungumza na waandishi wa habari wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa kiwanja hicho ili mmiliki wake apate haki.
Kwa mujibu wa maelezo ya familia na majirani eneo hili lililoko Buswelu “A” linamilikiwa na Mathias Lubango maarufu Kipara ambaye kwa sasa amekimbia makazi yake kutokana na hofu ya vitisho na kukamatwa mara kwa mara.
Mke wa Lubango anayefahamika kwa jina la Sharifa salehe amesema, eneo hilo walilinunua kwa Makoye Mshelela mwaka 2003 na mwaka 2015 eneo hilo likapimwa kupitia upimaji shirikishi hata hivyo baada ya barabara ya lami kujengwa inadaiwa watu kadhaa walianza kumzonga mmewe wakimtaka awauzie eneo hilo, mmoja wao akiwa mtumishi wa halmashauri.
Mama huyo anaeleza wamekuwa wakipokea nyaraka mbalimbali wakitakiwa kupisha eneo hilo nyaraka wa kwanza ukidai ni kupisha ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa, waraka wa pili ulidai eneo hilo ni hifadhi ya barabara, wa tatu ukiwa ni tangazo la kuuza kiwanja.
Akizungumza mara baada ya kusikiliza mgogoro huo uliowakutanisha walalamikaji pamoja na wataalamu wa idara ya ardhi wanaotuhumiwa, Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amir Mkalipa, amekiri kuufahamu mgogoro huo na kueleza hatua ambazo zitachukuliwa.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: