WASIMAMAZI WA UCHAGUZI WAJIVUE UANACHAMA WA VYAMA VYA SIASA -DKT ZAKIA
Автор: TZA MEDIA HUB
Загружено: 2025-07-15
Просмотров: 306
Maafisa wa uchaguzi nchini wametakiwa kuishi katika viapo vyao kwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, kutotoa taarifa yoyote ya uchaguzi kwa chombo chochote isipokuwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, na kujiondoa rasmi katika uanachama wa vyama vya siasa ili kudumisha uaminifu na usawa katika mchakato wa uchaguzi mkuu ujao.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Mheshimiwa Dkt. Zakia Abubakar, alipofungua rasmi mafunzo ya siku tatu ya utendaji kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wa ngazi ya jimbo katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Awali kaimu wa Mkurugenzi wa tume Huru ya uchaguzi Stanslaus Mwita amesema maafisa wote wamekula kiapo rasmi na kujaza fomu maalumu zinazowataka kujivua uanachama wa vyama vya siasa, kutunza siri za uchaguzi na kutotoa taarifa yoyote kwa chombo chochote isipokuwa kwa Tume au kwa kibali cha Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: