Huu ndio ukweli kilichotokea Kwale na Shumba Mjini - 1
Автор: Weyani Tv
Загружено: 2020-10-18
Просмотров: 75068
Kufuatia taarifa za mapigano baina ya wafuasi wa CCM wa kijiji cha Kwale na wafuasi wa ACT Wazalendo wa kijiji cha Shumba Mjini, wilaya ya Micheweni, kisiwani Pemba, ambayo yalipelekea watu kadhaa kujeruhiwa na kisha kuvamiwa kwa kijiji cha Shumba Mjini pekee na vyombo vya ulinzi na usalama, vilivyopiga mabomu, kuvunja majumba ya watu, kuchukuwa mali na fedha pamoja na kuwapiga na kuwakamata watu kadhaa, jioni ya saa 11:00 leo hii Jumapili ya tarehe 18 Oktoba 2020, Weyani TV imetembelea kijiji hicho kujionea hali ilivyo, ambapo imeshuhudia mitaa ikiwa mitupu na wanaume wengi wakiwa wamehama majumba yao kukimbilia maeneo mengine. Huu ndio ukweli wa tukio lenyewe kama linavyosimuliwa na mama ambaye ameomba asioneshwe sura yake.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: