SHIMMUTA YAUNGA MKONO KILIMO CHA MAZAO YA KIMKAKATI MOROGORO
Автор: RS MOROGORO
Загружено: 2025-12-05
Просмотров: 25
SHIMMUTA YAUNGA MKONO KILIMO CHA MAZAO YA KIMKAKATI MOROGORO
Shirikisho la Michezo la Taasisi, Makampuni na Mashirika (SHIMMUTA) limeunga mkono juhudi za Serikali ya Mkoa wa Morogoro katika kuendeleza kilimo cha mazao ya kimkakati, hususan zao la karafuu baada ya kununua miche ya mikarafuu yenye thamani ya shilingi milioni 2.
Hayo yamebainishwa Disemba 5, 2025 na Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Kamishna Mstaafu wa jeshi la Polisi Alhaji Dkt. Mussa Ali Mussa kwamba Serikali ya Mkoa huo inatekeleza programu ya kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kugawa na kupanda miche ya karafuu katika maeneo ya safu ya milima ya Uluguru.
Amesema programu hiyo ya kugawa bure miche kwa wananchi na wanafunzi wa kidato cha kwanza kutasaidia wanachi wa milima hiyo kutokata miti au misitu kwa kuwa baada ya kukua karafuu na kuanza kuvunwa itawaletea wananchi hao manufaa kiuchumi lakini pia kutunza mazingira ya milima hiyo.
Dkt. Mussa amesema kwa upande wa wanafunzi wa kidato cha kwanza pamoja na kutunza mazingira katika maeneo yao ya shule na nyumbani kwao itawasaidia kujiendeleza kielimu katika ngazi za juu na hivyo kuwapunguzia wazazi ama walezi wao kutafuta ada za shule.
"Tuna programu ya kuwagawia wanafunzi miche ya mikarafuu hususan wanafunzi wa kidato cha kwanza, ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae" amesema Dkt Mussa.
Aidha, Dkt. Mussa amebainisha kuwa kutokana na ukubwa wa Mkoa wa Morogoro na hali ya hewa ya mkoa huo inasaidia kustawisha zao hilo, Serikali ya Mkoa imejikita kuhakikisha Morogoro inakuwa kinara wa uzalishaji wa karafuu nchini na kupongeza jitihada hizo ambazo zinachochewa na na utoaji bure wa miche kwa wakulima ili kuongeza wigo wa uzalishaji.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Bw. Noel Kiunsi, amesema Shirikisho hilo limeamua kutoa fedha hizo kwa ajili ya kununua miche kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii na limekuwa likifanya hivyo mara nyingi kwa kutoa michango mbalimbali kwa taasisi tofauti.
Amesema, safari hii wamenunua miche ya karafuu yenye thamani ya shilingi milioni 2 na itagawiwa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kama mchango wao katika kuunga mkono programu ya Serikali ya Mkoa wa Morogoro ya kukuza kilimo cha mazao ya kimkakati likiwemo zao la karafuu.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha Amkeni, Bw. Azizi Omary, amemshukuru Katibu Tawala wa Mkoa kwa kuibua wazo hilo linloleta tija kwa jamii huku akibainisha kuwa mbali na kuinua kipato cha wananchi, miche hiyo itachangia pakubwa katika utunzaji wa mazingira kutokana na manufaa yake ya muda mrefu.
Mwisho.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: