Fafanuzi rahisi ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana - Kipindi cha Dhiki Kuu (Muhuri nne na Farasi wanne)
Автор: Bishop Dr. Fredrick Simon
Загружено: 2022-11-03
Просмотров: 2346
Fafanuzi rahisi ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana - Kipindi cha Dhiki Kuu (Muhuri nne na Farasi wanne) Na. Bishop Dr. Fredrick Simon
KIPINDI CHA DHIKI KUU
Dhiki kuu itagawanyika katika vipindi viwili.
Kipindi cha Kwanza – Miaka 3½
1. MAPIGO YA MUHURI SABA (6:1- 8:5)
i. Muhuri nne na farasi wanne (6:1-8).
Muhuri ya kwanza (6:1,2);
Farasi mweupe, naye aliyempanda ana Uta (Upinde), huonyesha kwamba ni Mpinga Kristo atakayekuja kama mtu wa amani, lakini anaiondoa hata ile amani ndogo iliyokuwepo duniani.
Kitabu cha Ufunuo wa Yohana kinawataja watu wawili waliopanda farasi weupe (dalili ya amani).
Mtu wa kwanza ana uta wa kuondoa amani, naye huyo ni mpinga Kristo.
Mtu wa pili hana uta, aitwa Mwaminifu na wa Kweli, huyo atakuja ili
auondoe uta, naye huyo ni Yesu Kristo – 19:11-16.
“Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.” Zaburi 46:9.
Muhuri ya Pili (6:3-4): Farasi mwekundu humaanisha vita ndani na nje ya nchi.
“Ninyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado” MATHAYO 24:6.
Muhuri ya Tatu (6:5,6): Farasi mweusi humaanisha njaa kali sana, maana bei ya chakula itapanda mno.
Muhuri ya Nne (6:7,8): Farasi wa kijivujivu humaanisha vifo kwa sababu ya njaa kali, wanyama wakali, maradhi, na kwa upanga EZEKIELI 14:21; ZEKARIA 6:2,3.
#ufunuowayohana #bishop #fredricksimon
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: