MIKOPO "YAVUNJA NDOA"-DIWANI ISEVYA
Автор: Cg Online Tv
Загружено: 2026-01-21
Просмотров: 65
Diwani wa Kata ya Isevya, Ramadhan Kapela, amezitaka taasisi zote za mikopo zinazofanya shughuli zake katika kata hiyo kuzingatia kikamilifu taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) za kutambua taarifa za mteja kabla ya kutoa mikopo, ili kuepuka kuwakopesha watu wenye madeni katika taasisi nyingine.
Akizungumza katika mkutano na wadau wa mikopo pamoja na viongozi kata hiyo, Kapela amesema kukiukwa kwa taratibu hizo kumesababisha ulimbikizaji wa madeni kwa baadhi ya wakopaji, hali iliyochangia kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati na kupelekea hasara kubwa kwao na kwa taasisi zinazowakopesha.
Ameongeza kuwa athari za hali hiyo zimekuwa kubwa kijamii na kiuchumi.
Kwa mujibu wa diwani huyo, baadhi ya wakopaji wamejikuta wakinyang’anywa mali zao na kuvunjika kwa ndoa.
Hata hivyo, watendaji wa taasisi za mikopo wameeleza changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa mikopo, wakibainisha kuwa baadhi ya wananchi wasio waaminifu wamekuwa wakiazimana mali kutoka kwa majirani zao ili kuwahadaa maafisa mikopo kuhusu mali wanazodai kuwa ni zao na kuzitumia kama dhamana.
“Unakuta mwanamke ameandika kuwa hana mume, lakini ikifika wakati wa kuchukua mali kutokana na mkopo kushindikana kulipwa, ghafla mume anajitokeza na kuanza malalamiko. Hii inaleta migogoro mikubwa katika familia na kwa taasisi za mikopo,” alisema Kapela. Alisema Elia William afisa mikopo wa taasisi mojawapo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: